Shule ya Msingi Mtonga iliyopo kata ya Mtonga imekamilisha Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Vitatu (03) vya Madarasa na Matundu ya Vyoo Sita (06). Mradi huo umegharimu jumla ya kiasi cha Shilingi Milioni Themanini na Nane na Laki Sita (88,600,000.00). kiasi hicho cha Fedha kilichotumika kimehusisha Ujenzi wa Vyumba Vitatu vya Madarasa, Matundu ya Vyoo Sita Pamoja na Madawati Arobaini na Tano kila Darasa moja limepata Madawati Kumi na Tano.
Fedha zote za Mradi zilizotumika zilimetolewa na Serikali kuu kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Awali na Msingi hapa Nchini (BOOST) katika Mwaka wa Fedha 2024/ 2025.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.