Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi awataka Watendaji ngazi ya Kata na Mitaa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato ya Halamshauri ya Mji wa Korogwe. Bi. Zahara Msangi ameyasema hayo katika kikao kazi na Menejimenti, Watendaji Kata na Mitaa kilichofanyika Novemba 21, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe.
Aidha Bi. Zahara Msangi amewaagiza Watendaji hao kufahamu biashara zinazofanyika katika Kata na Mitaa wanayofanyia kazi ili kurahisisha ukusanyi wa ushuru wa huduma (Service Leavy). Pia amewataka Watedaji kuandaa mikakati madhubuti ya ukusanyaji wa mapato kwani ushuru huo wa huduma unapopatikana utasaidia kuboresha huduma za afya,barabara, ukusanyaji taka na maendeleo ya Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.