Timu ya Kampeni ya Chanjo ya Uviko -19 yatembelea Magereza
Wafungwa kutoka Gereza la Wilaya ya Korogwe pamoja na Gereza la Kwamngumi yaliyopo katika Mji wa Korogwe wamepatiwa Chanjo ya Uviko -19 ikiwa ni jitihada za Serikali kuyafikia makundi mbalimbali kwa lengo la kuwaelimisha pamoja na kuwahamasisha ili wapate Chanjo ya Uviko -19. Zoezi la kuwapatia Chanjo Wafungwa hao limefanyika Oktoba 03, mwaka huu ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya utoaji wa Chanjo ya Uviko -19 Nyumba kwa Nyumba.
“Natoa pongezi kwa Serikali kwa kujumuisha Magereza katika mpango wa kupatiwa Chanjo ya Uviko -19, Magereza pia ni sehemu ya mkusanyiko wa watu” alisema SSP. Cristopher Mwenda ambaye ni Mkuu wa Gereza la Kwamngumi. SSP. Mwenda alifafanua kuwa Wafungwa ni sehemu ya jamii hivyo Timu nyingine za Wataalamu wa Afya kutoka Serikalini zinakaribishwa kutoa elimu pamoja na matibabu ya magojwa mengine.
Nae Dkt. Salma Sued ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alitoa shukrani kwa Uongozi wa Gereza la Wilaya ya Korogwe pamoja na Gereza la Kwamngumi kwa kutoa kibali cha ruhusa ya kutoa hamasa pamoja na Chanjo ya Uviko -19 kwa Wafungwa. Dkt. Sued Alifafanua kuwa utamaduni wa kuwatembelea Wafungwa waliopo katika Magereza hayo utakuwa endelevu kwa lengo la kuwapatia elimu ya afya pamoja na matibabu ya magojwa mbalimbali.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.