Mratibu wa mradi wa TACTIC Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhandisi Bw. Charles Kamugisha, Mhandisi Bw. Zakayo Magoro ambaye ni Meneja wa TARURA, Wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji Korogwe Pamoja na Wakandarasi wanaotazamiwa kuomba Zabuni juu ya mradi wa TACTIC wametembelea maeneo ambayo Barabara zitajengwa kwa kiwango cha Lami.
Miradi iliyotembelewa na Wakandarasi Pamoja na timu nzima ya wataalamu ni Barabara ya John Kijazi - Modern Market, Brabara ya Bagamoyo - Mgombezi – Kibo na Barabara ya NMB – Magunga kwa ujumla zote zina urefu wa Km. 10.2 pamoja na Mifereji ya maji (Storm water drain) ambayo ni Mountain View – Muzdalfa, TTC – Mbeza na mfereji wa Sokoni - Mbeza yenye urefu wa Km 2. Ziara hiyo ilifanyika Febuari 25, 2025 kwenye maeneo ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.