Ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Mbeza Mazoezi wasonga mbele
Mpaka kufikia Mei 13, Mwaka huu (2024), Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Mbeza Mazoezi, iliyopo Kata ya Manundu katika Mji wa Korogwe umefikia kwenye hatua ya Renta. Mradi huo wa Vyumba Viwili vya Madarasa unatekelezwa kwa fedha kiasi cha Shilingi Milioni Arobaini. Kiasi hicho cha fedha kilitolewa na Serikali Kuu kwa lengo la uboreshaji wa Sekta ya Elimu hapa Nchini.
Ujenzi huo wa Vyumba Viwili vya Madarasa unakwenda sambamba na Ujenzi wa Matundu ya Vyoo Ishirini na Tano. Matundu hayo Ishirini na Tano ya Vyoo yanatekelezwa kwa Kiasi cha Shilingi Milioni Ishirini na Nane. Kiasi hicho cha fedha pia kilitolewa na Serikali Kuu. Kukamilika kwa Mradi huo wa Vyumba vya Madarasa pamoja na Matundu ya Vyoo utasaidia Wanafunzi kuwa na Idadi ya kutosha ya Vyumba vya Madarsa pamoja na Matundu ya Vyoo na kupelekea Shule hiyo kuwavutia Wanafunzi wengi kujiunga na Shule hiyo.
Akizungumzia utekelezaji wa Mradi huo wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa pamoja na Matundu ya Vyoo katika Shule ya Msingi Mbeza Mazoezi, Bi. Mwashabani Mrope ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema “ Natoa shukrani za dhati kwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa pamoja na Matundu ya Vyoo, Kukamilika kwa Mradi huu kutasaidia uboreshaji wa Elimu katika Kata ya Manundu”.
Kwa upande mwengine, Bi. Mwashabani Mrope alitoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rajabu Mzige ambaye ni Diwani wa Kata ya Manundu, Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mbeza na Wananchi kwa ujumla kwa kushirikiana vyema na Wataalamu wa Halmshauri ya Mji wa Korogwe katika usimamizi wa Mradi ili uweze kukamilika kwa wakati. Mradi wa Ujenzi katika Shule ya Msingi Mbeza Mazoezi utekelezaji wake ulianza Mwenzi Aprili, 2024 na unatarajiwa ifikapo Mwezi Juni 2024, Mradi wote wa Ujenzi uwe umekamilika.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.