Umaliziaji wa Vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya Walimu katika Shule ya Msingi New Korogwe katika kata ya Majengo Halmashauri ya Mji wa Korogwe umefikia hatua ya upakaji rangi, uwekaji wa marumaru na kufanya skiming. Umaliziaji huo wa Vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja umegharimu kiasi cha Shilingi Milioni Ishirini na nane laki sita sitini na mbili elfu na mia tano (28,662,500) fedha zote hizo zimetolewa na Mradi wa Shule bora, Mfuko wa jimbo Pamoja na Serikali kuu. Fedha zote zimetolewa kwa ajili ya umaliziaji wa Madarasa hayo mawili Pamoja na ofisi moja”. Kazi na utu tunasonga mbele”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.