Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mheshimiwa William Mwakilema azindua kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Uzinduzi huo umefanyika Novemba 25, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Mwakilema amewataka viongozi wa viongozi wa dini kuombea na kuhamasisha amani kwa Taifa.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Zahara Msangi amemshuruku Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha wanawake kupata mikopo ya asilimia 10 ambayo inapunguza kasi ya ukatili kwa wanawake. Aidha amewataka wanawake kuhimiza watoto wakike kujiunga katika vikundi ili kupokea mikopo ya asilimia 10 na kuanzisha miradi itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi na kupunguza ukatili.
Aidha Bi. Zahara Msangi amewapongeza wananchi wa Korogwe kwa kuwa na mshikamano na kufanya kazi kwa bidii. Pia amewaahidi wananchi wa Korogwe kutoa ushirikiano huo kwa kuwa na upendo kuepuka vitendo vya ukatili.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.