Vikundi 09 vilivyoidhinishiwa kupatiwa Mikopo ya Asilimia kumi katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe vimepatiwa Mafunzo ya Jinsi ya usimamizi mzuri wa Fedha katika vikundi vyao. Lengo kuu ya Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanakikundi ambao watakaopatiwa Mikopo ya Asilimia10% ili wawaze kujikomboa kiuchumi.Wawezeshaji wa Mafunzo hayo walikuwa ni Maafisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Wanufaika wa mikopo ya Asilimia kumi ni Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.Mafunzo hayo yalifanyika Mei 03, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe yanatarajia kumalizika Mei 06, 2025.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.