Vikundi vilivyoidhinishwa kupata mikopo vyapatiwa mafunzo
Vikundi 40 vilivyoidhinishwa kupatiwa mikopo ya asilimia kumi katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe vimepatiwa mafunzo ya jinsi ya usimamizi mzuri wa fedha katika vikundi vyao ili vikundi hivyo viweze kutimiza lengo la kuwakomboa wananchi kiuchumi. Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni Maafisa maendeleo wa Jamii wa Mji wa Korogwe pamoja na Maafisa wa Takukuru wa Wilaya ya Korogwe. Mafunzo hayo yalifanyika Desemba 11, 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na yanatarajiwa kumalizika Desemba 12, 2024.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.