Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Charles James Mtali akiamabatana na Maafisa maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe ametembelea Vikundi vilivyonufaika na mikopo ya asilimia kumi kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025. Matembezi hayo yalifanyika Septemba 19, 2025 (Mwaka huu) katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Vikundi vilivyotembelewa na Afisa huyo ni kikundi cha Wanawake cha UWAMSA kinachojishughulisha na ufyatuaji wa matofali ya saruji na kiliingiziwa kiasi cha Shilingi Milioni 6,000,000. Kikundi hicho kipo Mtaa wa Msambiazi kata ya Mtonga. Kikundi cha pili ni kikundi cha Vijana Winners Group kilichopo Mtaa wa Old Korogwe kata ya Old Korogwe Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Kikundi hicho kinajishughulisha na uzalishaji wa majiko yanayotumia nishati safi Pamoja na uuzaji wa makaa ya mawe. Lengo la kikundi hicho ni kuinua kipato na kujenga mshikamano na kina jumla ya wanachama watano , wanaume wanne na mwanamke mmoja. Kikundi hicho kiliingiziwa jumla ya fedha Shilingi Milioni 13,000,000 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Kikundi kingine kilicho tembelewa ni kikundi cha Bw. Mwanga Ntandu mwenye ulemavu wa macho anayeishi kata ya Masuguru.
Bw. Ntandu anajishughulisha na usafirishaji wa abiria kwa njia ya Bajaji aliyoipata kutokana na mkopo wa asilimia 2% ya mapato ya ndani ya Halmashauri. Bw. Ntandu aliingiziwa kiasi cha Shilingi cha Milioni 11,000,000.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.