Mratibu wa Dawati la jinsia Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Herieth Sanga kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope akiambatana na Maafisa Maendeleo ya Jamii Pamoja na Ustawi wa jamii kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe ametembelea Vikundi vilivyonufaika na mikopo ya asilimia kumi kwa mwaka wa fedha 2024/2025.Vikundi hivyo vimetembelewa leo Septemba17, 2025 (Mwaka huu) katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Vikundi vilivyotembelewa na maafisa hao ni Pamoja na Kikundi cha Wanawake cha UWAMSA kilichopo katika Mtaa wa Msambiazi kata ya Mtonga kiliingiziwa Shilingi Milioni 6,000,000. Kikundi hicho kinajihusisha na uzalishaji wa matofali ya sementi. Kikundi cha pili ni kikundi cha Vijana cha Kwakombokuku kinachojishughulisha na ufugaji wa kuku wa nyama na wa mayai. Kikundi hicho kiliingiziwa jumla ya Shilingi Milioni 4,000,000.
Mwisho walimtembelea Bw. Mwanga Ntandu mwenye ulemavu wa macho anayeishi kata ya Masuguru. Bw. Ntandu anajishughulisha na usafirishaji wa abiria kwa kutumia bajaji aliyoinunua kutoka na mkopo wa asilimia 2% ya Watu wenye ulemavu kiasi cha Shilingi Milioni 11,000,000. Fedha zote zimetolewa na Halmashauri ya Mji wa Korogwe kupitia mapato ya ndani.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.