Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Korogwe Mjini Bi. Mwashabani Mrope amewataka Viongozi wa vyama vya Siasa kuhamasisha Wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye zoezi la Uboreshaji wa Daftarila kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili pamoja na kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate sifa ya kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba Mwaka huu (2025 na Orodha ya awali ya wananchi waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura itabandikwa kweye Vituo vyote vilivyotumika kwenye uboreshaji wa awamu ya kwanza. Bi. Mwashabani Mrope alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha wadau wa Uchaguzi kilichowakutanisha vyama mbalimbali vya Siasa kwa lengo la kujadili uwepo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika Jimbo la Korogwe Mjini kwa awamu ya pili. Kikao hicho kilifanyika Mei 08, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika awamu ya pili linatarajiwa kuanza Mei 16, mwaka huu (2025) na kumalizika Mei 22, mwaka huu (2025. Vituo vyote vitafunguliwa kuanzia Saa 2: 00 Asubuhi na kufungwa Saa 12: 00 Jioni.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.