Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki waapishwa
Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki kwaajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura katika Jimbo la Korogwe Mjini wameapishwa na kupewa mafunzo ya namna ya uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kwaajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba, 2025. Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki takribani 204 waliapa mbele ya Afisa Mwandikishaji Msaidizi wa Jimbo la Korogwe Mjini Bi. Mwajabu Mkindi. Kiapo hicho pamoja na mafunzo kilifanyika Februari 10, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Mafunzo ya namna ya uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kwa Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki yamepangwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Februari 10 hadi 11, 2025. Mafunzo hayo yameratibiwa na Afisa Mwandikishaji Msaidizi Jimbo la Korogwe Mjini kwa kushirikiana na Maafisa kutoka Tume huru ya Taifa ya uchaguzi nchini Tanzania.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.