Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki kwaajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili katika Jimbo la Korogwe Mjini wameapishwa na kupewa mafunzo jinsi ya uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kwaajili ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Mwezi Oktoba, Mwaka huu (2025). Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometri wapatao 72 waliapa mbele ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Korogwe Mjini Bi. Mwashabani Mrope. Kiapo hicho na mafunzo yalifanyika Mei 14 Mwaka huu (2025) katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Mafunzo ya namna ya Uboreshaji wa taarifa za wapiga kura kwa Waandishi wasaidizi na wale waendesha vifaa vya bayometriki yamefanyika kwa Siku moja Mei 14, 2025. Mafunzo hayo ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura kwa awamu ya pili linahusu shughuli zifuatazo kuandikisha wapiga kura wapya waliotimiza miaka 18 na wale watakaotimiza miaka 18 mwezi Oktoba mwaka huu , kutoa kadi mpya kwa wale waliopoteza kadi au kadi zao zimeharibika, kuboresha au kurekibisha taarifa za wapiga kura ambao taarifa zao zimekosewa. Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 200: Asubuhi na kufungwa Saa 12: Jioni. “Kujiandikisha kuwa Mpiga
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.