Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele amewataka Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki katika Jimbo la Korogwe Mjini kufanya kazi kwa uadilifu pamoja na kuzingatia kanuni na taratibu zote zilizoainishwa katika miongozo wakati wa utekelezaji wa zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025. Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele alitoa kauli hiyo Februari 10, Mwaka huu (2025) wakati akikagua mafunzo kwa vitendo kwa Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.