Wadau wa elimu Mji wa Korogwe wakutana kujadili uboreshaji wa elimu
Wadau wa elimu katika Mji wa Korogwe wamekutana katika kikao maalum kinanchofanyika kila mwaka, kikao ambacho huratibiwa na Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa lengo la kujadili namna ya uboreshaji wa Sekta ya elimu katika Mji wa Korogwe. Kikao hicho kilichowakutanisha Wadau wa elimu kutoka ngazi ya Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Taasisi Binafsi, Taasisi za Serikali pamoja na Wadau mbalimbali kilifanyika Machi 15, mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Wadau wote wa elimu tushikamane kwa dhati kwenda kuboresha elimu kwa maendeleo ya Mji wetu wa Korogwe” alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati wa mkutano wa wadau wa elimu. Mhe. Komba alifafanua zaidi kuwa ili Mji wa Korogwe uweze kusonga mbele katika Sekta ya elimu ni vyema kila mdau wa elimu kuainisha changamoto zilizopo mashuleni na kufanya majadiliano kwa kina pamoja na kutathimini namna gani changamoto hizo zinaweza kutatuliwa.
Kwa upande mwengine, Wadau mbalimbali walioshiriki katika kikao hicho cha elimu walitoa mapendekezo yao kuwa ili Sekta ya elimu iweze kusonga mbele ni vyema kukaanzishwa utaratibu wa wanafunzi ukupata chakula cha mchana shuleni. Mapendekezo mengine yaliyotolewa ni pamoja utoaji wa motisha kwa walimu pamoja na wanafunzi walifanya vizuri katika masomo yao ili waweze kuongeza jitihada katika masomo.
Katika hatua nyengine, Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe pamoja na Ndugu Nicodemus Bei ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe walikabidhi zawadi kwa shule pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihadi ya kumaliza elimu ya Darasa la Saba pamoja na Kidato cha Nne kwa mwaka 2021 kwa Shule za Serikali pamoja na Shule za Taasisi Binafsi.
Nao Walimu waliokabidhiwa zawadi kwa niaba ya Shule zao pamoja na Wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kumaliza masomo kwa mwaka 2021 walitoa shukrani zao kwa Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kuwapatia zawadi na kuahidi kuwa wataongeza bidii katika ufundishaji na pamoja na kuwahamsisha wanafuzi wasome kwa bidiii ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mitihani ijayo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.