Wadau wa uchaguzi Mji wa Korogwe wapigwa msasa
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope ametoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. Bi. Mwashabani alitoa maelekezo hayo katika Kikao maalumu kilichokutanisha Wadau mbalimbali wa Uchaguzi kwa lengo la kupeana maelekezo ya namna uchaguzi utakavyotekelezwa. Kikao hicho kilifanyika Septemba 26, Mwaka huu katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Kikao hicho kilichoangazia taratibu za ushiriki wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kilishirikisha Wadau kutoka makundi mbalimbali. Wadau hao ni pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Kamati ya Amani ya Wilaya, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wazee, Watendaji wa Kata pamoja na Mitaa.
Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ulitangazwa rasmi Agosti 15, Mwaka huu (2024) na Waziri wa Tamisemi Mhe. Mohamed Mchengerwa, na unatarajiwa kukamilika Novemba 27, Mwaka huu (2024) ambayo ndiyo itakuwa siku rasmi ya upigaji wa Kura kwa ajili ya kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.