Wafanyabiashara Ndogondogo, Mawakala wa Babasi wajitokeza kupata Chanjo ya Uviko -19
Wafanyabiashara ndogondogo pamoja na Mawakala wa mabasi yanayokwenda Mikoani katika Kituo cha Mabasi cha John Kijazi kilichopo Mji wa Korogwe wamejitokeza kupatiwa Chanjo ya Uviko -19. Timu ya Kampeni ya Mpango Harakishi na Shirikishi wa Chanjo ya Uviko -19 ilitembelea Kituo cha mabasi cha John Kijazi Septemba 29, mwaka huu kwa lengo la kuwaelimisha pamoja na kuwahamasisha Wananchi wapate Chanjo ya Uviko -19.
“Namiomba kila mmoja wetu aliyepata elimu ya umuhimu wa Chanjo ya Uviko -19 na kuelimika, aende akamuelimishe na mtu mwingine” alisema Dkt. Salma Sued ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati akizungumza na Wafanyabiashara Ndogondogo pamoja na Mawakala wa Mabasi katika Kituo cha Mabasi cha John Kijazi. Dkt. Sued alisisitiza kwa kusema “Wananchi tujiepushe na propaganda za mitandao ya kijamii, Chanjo hii ni salama na haima madhara yoyote kwa matumizi ya binadamu”
Nae Ndugu Maurice Kinyashi ambaye ni Meneja wa Kituo cha Mabasi cha John Kijazi kilichopo Mji wa Korogwe alisema “natoa shukrani za dhati kwa Timu ya Kampeni ya Mpango Harakishi na Shirikishi wa Chanjo ya Uviko -19 kututembelea na kutupatia elimu ya chanjo, tumehamasika na tutakwenda kuwahamasisha wananchi wengine”.
Katika hatua nyengine, Timu ya Kampeni pia ilitembelea Kituo cha Mabasi cha Zamani (Stendi ya Zamani) katika Mji wa Korogwe kwa lengo la kutoa elimu pamoja na kuwahamasisha Wafanyabiashara Ndogondogo na Wananchi wote kwa ujumla wapate Chanjo ya Uviko -19.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.