Wafanyabiashara wa soko la Manundu lilipo katika Kata ya Manundu Halmashauri ya Mji Korogwe wafurahishswa na utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe aliyewatembelea na kuzungumza nao Disemba 01, 2025. kikao hicho kilikuwa na lengo la kuboresha soko kwa manufaa ya Wafanyabiashara na Wananchi wa Korogwe.
Katika kikao hicho Bi. Zahara Msangi amewataka Wafanyabiashara kuwa na umoja kama siafu ili kufika salama katika kuendeleza Korogwe yetu. Pia amewataka kubuni namna bora ya kueendesha biashara zao na kuwataka kuzungumza changamoto wanazopata katika ulipaji kodi na ushuru wa huduma katika Halmashauri.
Naye Katibu wa soko hilo Bw. Ramadhani Kusaka ametoa pongezi hizo kwa Mkurugenzi katika kikao hicho na kumshukuru kwa kutenga muda na kuwasiliza. Pia ameleeza kuwa watatoa ushirikiano katika kuhakikisha Wafanyabiashara hao wanakata leseni na kutoa ushuru kwa wakati.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.