Wageni wanaendelea kujitokeza kwa wingi katika Banda la Halmashauri ya Mji wa Korogwe kuona Mazao mbalimbali yaliyoandaliwa na Wataalamu wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi zenye ubora wa hali ya juu katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuanzia Agosti 1 hadi Agosti 8,2025. Banda la Halmashauri ya Mji wa Korogwe lina Mazao ya Kilimo Mifugo na Uvuvi yakiwemo Mahindi, Pilipili,Kabichi, Nyanyamaji, Pilipili Hoho Pilipili, pamoja na Bamia na matembele. Kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane kwa Mwaka huu yanasema”Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.