Wajumbe Waazimia kuboresha Lishe ya Mama Wajawazito na Watoto Shuleni
Wajumbe wa Kamati ya Lishe katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe wameazimia kuboresha Lishe ya Mama Wajawazito pamoja na Watoto Shuleni. Mama Wajawazito wataboreshewa Lishe kwa watapatiwa Elimu ya Lishe pamoja na Vidonge vya kuongeza Damu wanapohudhuria Kliniki. Watoto Shuleni pia wataboreshewa Lishe kwa kupatiwa chakula cha mchana. Maazimio hayo yalitolewa Agosti 21, Mwaka huu (2024) katika Kikao cha Kamati ya Lishe kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.