Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bw. Elinaa Kivaya akiambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo watembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 katika Halmashauri ikiwa ni utaratibu wa kila wiki katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Ziara hiyo imefanyika Disemba 11, 2025 katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ukamilishaji wa maabara katika shule ya Sekondari Joeli Bendera, Kwamndolwa, Kilole, Kimweri na Ngombezi, Ukamilishaji wa chumba 1 cha darasa katika shule ya msingi New korogwe na Matondoro pamoja na Ukamilishaji wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya msingi Kwamdulu.
Katika Kikao cha majumuisho ya Ziara ya kutembelea miradi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kutoa ushauri utakaowezesha ubora wa ukamilishaji wa miradi inayotekelezwa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Wazabuni wanalipwa kwa wakati ili kutoa huduma katika miradi inayoendelea
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.