Mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa somo la Hisabati yanaratibiwa na progranmu ya SHULE BORA( Shule ni programu ya elimu ya serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa mfuko wa UK aid inayolenga kuinua ubora, ushirikishwaji na mazingira salama ya kujifunzia kwa shule za msingi za serikali nchini) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Korogwe yametolewa kwa Walimu wa shule za msingi Halmashauri ya Mji Korogwe.
Mafunzo ya siku 4 ya kuwajengea uwezo walimu 41 wa somo la Hisabati yalianza Novemba 21, 2025 na kumalizika Novemba 24, 2025, mafunzo yamefanyika shule ya msingi Boma iliyopo Kata ya Majengo Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Mratibu wa SHULE BORA Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Amina Nyangasa kwa kushirikiana na wawezeshaji (Walimu mahiri wa Hisabati) wamewezesha walimu katika mahiri mbalimbali ikiwemo mahiri ya Jometri,Aljebra,Vipimo na namna ya kutatua changamoto wanazokutana nazo walimu wa somo la Hisabati katika ufundishaji na ujifunzaji.
Aidha Bw. LazaroThobias mwenzeshaji wa mafunzno hayo kutoka shule ya msingi Lwengera Darajani aliwawezesha walimu kufahamu namna ya uandishi wa rejea, kuandaa zana, kuandaa maazimio na maandalio ya somo. Naye Bw. Rajabu S. Mbalu mwezeshaji kutoka shule ya msingi Mgombezi aliwawezesha walimu kutumia teknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji wa mahiri ya Hisabati.
Mshiriki Bi. Zaina Mbuji amemshuruku Mkurugenzni wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Zahara Msangi kwa kuruhusu mafunzo hayo kufanyika kwani katika mafunzo hayo wameweza kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo, kuoresha ujifunzaji na ujifunzaji,kutumia mbinu na zana stahiki pamoja na kuimarisha mtazamo chanya kuhusu ujifunzaji na ufundishaji wa umahiri wa somo la Hisabati.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.