Kwamujibu wa afisa elimu sekondari Bi…kwa niaba ya mkurugenzi wa mji wa Korogwe, jumla ya wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu ni 1594 wanaume wakiwa 828 na wanawake 766.Jumla hiyo ni sawa na ongezeko la wanafunzi 294 mwaka jana ambapo walichaguliwa 1300.
Kutokana na ongezeko la ufaulu wanafunzi hao watajiunga kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza wameanza 1422 na waliobaki 172 watajiunga kabla ya mwezi wa tatu mwaka huu.Hali hii imejitokeza hasa kwa sababu ya upungufu wa vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule za sekondari za Korogwe mji.Lakini hata hivyo kuna jitihada mahususi zinaendelea za ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule za sekondari Kilole,Kimweri na semkiwa na vitakuwa tayari kabla ya mwezi wa tatu.
Serekali ya awamu ya tano ikiongozwa na Dr. John Pombe Magufuli inafanya jitihada kubwa kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu kama ipasavyo mathalani kwa kutoa elimu bila malipo na ujenzi wa miundo mbinu wezeshi kwa mfano maabara na vyumba vya madarasa.Hivyo ni rai kwa wazazi wote washirikiane na serekali kuhakikisha wanahimiza watoto wao kuhudhuria shuleni.Elimu ndio jambo pekee litakalomwezesha taifa hili kufikia uchumi wa viwanda kama ilivyo kauli mbiu yetu kwa sasa.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.