Wananchi wa Korogwe wajitokeza kwa wingi kwenye Mdahalo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Wananchi kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe pamoja na Wilaya ya Korogwe wamejitokeza kwa wingi katika Mdahalo unaohusu Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mdahalo huo ulijikita Zaidi kuzungumzia matunda ya Muungano katika kipindi cha Miaka 60 kwa Wananchi wa pande zote mbili za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Mdahalo huo ulifanyika Aprili 25, Mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe huku Mgeni Rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema.
Kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzbibar zinatarajiwa kufanyika Aprili 26, Mwaka huu (2024) Mkoani Dodoma huku Mgeni Rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ya Miaka 60 ya Muungano ni: Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.