Mratibu wa dawati la mtoto Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Amina Fundi akiambatana na wataalamu wa maendeleo ya Jamii ametembelea jukwaa la uwezeshaji wanawake kiu uchumi. Lengo kuu ya ziara hiyo ni kuwajengea uwezo wanajukwaa hao, pamoja na kutoa elimu juu ya maswala ya ukatili wa kijinsia kwa wanajukwaa hao. Ziara hiyo ilifanyika katika kata ya Mtonga Novemba 6,2025. Bi. Amina Fundi aliendelea kusisitiza wanajukwaa hao kuandaa miradi yenye tija ili kuweza kujiinua kiuchumi.
Naye Bi. Rahma Kahelo ambaye ni mratibu wa dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi aliwaomba, wanawake hao kuwa chachu ya kuhamasisha na kuwa elimisha wanawake wengine kujiunga na jukwaa hilo. Vikundi vilivyotembelewa ni pamoja na kikundi cha Hekima, Women power na Kiwam vinavyojishughulisha na ufugaji wa kuku wa nyama .Kwaupande mwingine Bi. Rehema Rashidi aliishukuru Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kuwapatia mikopo ya asilimia kumi yanayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri, kuendelea kuitoa kwani ina manufaa makubwa kwetu sisi na kwa jamii nzima.

Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.