Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. William Mwakilema amewataka Wananchi walionufaika na mkopo wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe unaotokana na mapato ya ndani ya asilimia kumi kurejesha mkopo huo kwa wakati ili kunufaisha Wananchi wengine, pia alisisitiza kufuata sheria za Barabarani wakati wakiendesha vyombo vya moto ili vyombo hivyo vidumu muda mrefu.
Mh. Mwakilema alitoa nasaha hiyo Septemba 25, 2025 katika hafla ya kukabidhi hundi ya mkopo yenye thamani ya shilingi Milioni mia moja ishirini na saba laki saba hamsini na tano elfu mia moja kumi na tisa na senti tisini (127,755,119.90) kwa vikundi kumi na saba (17) vya Wanawake, Vijana, na Watu wenye ulemavu katika kipindi cha robo ya Nne ya mwaka wa fedha 2024/2025.Hafla hiyo imefanyika kweye Mtaa wa Manzese kata ya Bagamoyo Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope alisema” kupitia utoaji wa mkopo wa asilimia kumi tumeweza kupunguza tatizo la ajira katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mikopo hii imeenda kupunguza kabisa utegemezi katika familia zao kupitia mkopo asilimia kumi. Kwa upande Wanawake imetengwa asilimia 4%, Vijana asilimia 4%, Pamoja na Watu wenye ulemavu asilimia 2%, jumla inakamilsha asilimia 10% kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.