-
@samia_suluhu_hassan
@ikulu_mawasiliano
@owm_tz
@ortamisemi
@urtmof
@maendeleoyajamii
@rc_tanga_official
@batilda.burian
@dc_korogwe
@ms_rajabu
@zahmsangi
Mratibu wa Mikopo asilimia 10 kwa wanawake, Vijana na walemavu Bi.Rahma Kahelo aongoza mafunzo ya mbinu mkakati kiuchumi kwa wanuafaika wa mikopo. Wanufaika hao wamepatiwa mafunzo ya siku tatu kuanzia Disemba 2, 2025 na kuendelea Disemba 5 Hadi 6, 2025. Mafunzo hayo ya siku tatu yametolewa katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe.
Wanavikundi walipatiwa mafunzo ya ujasiriamali, mbinu za utunzaji fedha, kufungua biashara na nembo za kibiashara, umuhimu wa utunzaji kumbukumbu pamoja kupambana na Rushwa. Mafunzo hayo wezeshi yatawasaidia katika nyanja mbalimbali katika miradi yao
Naye Msaidizi wa Mratibu wa mikopo asilimia 10 Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Blandina Mhina aliwashauri vikundi kuachana na mikopo inayopelekea kuaibishwa mitaani na kuzingatia kanuni na taratibu walizowekewa ili kujikwamua kiuchumi kupitia fedha za asilimia 10 za Mapato ya ndani na marejesho zinazotolewa na Halmashauri.
Mwenyekiti wa Wanuafaika mikopo asilimia 10 Bw. Fadhili Ally Mohammed ameishukuru Halmashauri ya Mji Korogwe kwa kuwapatia mikopo kwani itawakomboa na kustawisha familia zao na Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.