Wasimamizi wa uchaguzi Jimbo la Korogwe Mjini wapewa mafunzo
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Korogwe Mjini Ndugu Nicodemus Bei ametoa mafunzo kwa wasimamizi takribani 568 wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumanato, Oktoba 28, mwaka huu. Mafunzo hayo yalioambatana pamoja na kiapo cha uchaguzi yamefanyika Oktoba 25, mwaka huu katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Mafunzo hayo ya uchaguzi yalitolewa kwa lengo la kuwafunda wafanyakazi mbalimbali ambao wanatarajiwa kushiriki kwenye kazi za uchaguzi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi. Wafanyakazi hao ni pamoja Wasimamizi wakuu 142, Wasimamizi wasaidizi 284, pamoja na Makarani waongozaji 142. Kuhusu mgawanyo wa maeneo, Jimbo la Korogwe Mjini limegawanywa katika Kata Kumi na Moja huku likiwa na idadi ya vituo vya kupigia kura 142.
“Wasimamizi wa uchaguzi mnatakiwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa, uadilifu pamoja na kuzingatia kanuni na taratibu zote za uchaguzi” Ndugu Nicodemus Bie ambaye ni Msimamizi wa Jimbo la Korogwe Mjini alisema. Ndugu Bei aliendelea kusisitiza kwa kusema “ “wasimamizi wa uchaguzi mnatakiwa kujiepusha na itikadi za chama chochote cha siasa wakati wa kufanya kazi na yeyote atakayekiuka atachukuliwa hatua kali za kisheria”.
Kwa upande mwingine, washiriki wote mafunzo baada ya kula kiapo cha uchaguzi waliahidi kuwa watafanya kazi kwa uadilifu mkubwa wakizingatia kanuni na taratibu zote za uchaguzi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.