Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura waapishwa
Wasimamizi wakuuu pamoja na Wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 wameapishwa na kupewa mafunzo ya taratibu za usimamizi wa vituo vya kupigia kura. Wasimamizi hao wa vituo vya kupigia kura katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe waliapa mbele ya Mhe. Sikitu Mwalusamba ambaye ni Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Korogwe. Kiapo hicho pamoja na mafunzo kilifanyika Novemba 23, Mwaka huu (2024) katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.