Wasimamazi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata Halmashauri ya Mji wa Korogwe wameapishwa na kupewa mafunzo kwa kujengewa uwezo na namna ya kufuata miongozo, kanuni, taratibu pamoja na Sheria zinazotolewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025 (Mwaka huu). Wasimamizi hao wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe wameapa Mbele ya Mh. Nelusigwe J. Mwalyanga Hakimu Mkuu wa Mahakama ya mwanzo Old Korogwe katika Wilaya ya Korogwe. Kiapo hicho pamaja na mafunzo yamefanyika Agosti 4, (Mwaka huu) 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Wasimamizi wapatao 22 wa uchaguzi ngazi ya kata waliapa Mbele ya Mh. Hakimu Nelusigwe Mwalyanga. Mafunzo hayo yanatarajia kudumu kwa Siku 3 kuanzia Agosti 4 hadi Agosti 6 ,2025 (Mwaka huu).
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.