Mkuu wa Idara ya Kilmo, Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Ramadhani Sekija akiwa na Afisa Lishe Bw. Zabron Osima katika Banda la Maonesho ya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakitoa Elimu ya mazao mbalimbali likiwemo zao la Mkonge linalolimwa kwa wingi Korogwe Mji. Bw. Sekija alitoa Elimu hiyo Agosti 4, 2025 katika Banda la Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa Wageni waliofika kujionea zao la Mkonge linavyotekelezwa Korogwe Mji. Maonesho hayo yanafanyika ndani ya Mkoa wa Morogoro katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere kuanzia Agosti 1 hadi Agosti 8, 2025.
Kwa upande mwingine Bw. Zabron Osima akifafanua suala la kuboresha lishe kwa Mama wajawazito pamoja na Watoto wadogo walio na umri chini ya miaka mitano ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa Watoto. Bw Osima aliwaeleza wageni waliofika katika Banda kuwa kwa sasa kuna Changa moto ya uzito uliopitiliza na Lishe duni kwa baadhi ya makundi husika. Bw Osima pia alisema ni vema wananchi wajitokeze kupima mara kwa mara Magonjwa yasiyoambukiza ili kuondokana na uzito uliopitiliza na kujikinga na Magonjwa ya Kisukari, na Shinikizo (Presha).
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.