Watendaji wa Vijiji watakiwa kusaidia kutatua migogoro ya ardhi
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kalist Lazaro Bukhay amewataka Watendaji wa Vijiji kusaidia kutatua migogoro ya ardhi ili kupunguza changamoto za migogoro ya ardhi inayojitokeza katika jamii. Maelekezo hayo aliyatoa Novemba 02, mwaka huu wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani cha Papo kwa Papo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Kikao hicho cha Baraza la Madiwani kilifanyika kwa lengo la kuhitimisha Robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2021/22.
“Migogoro midogo midogo Watendaji wanatakiwa kuitatua kabla ya kufika kwa Mkuu wa Wilaya “alisema Mhe. Kalist Lazaro Bukhay wakati wa Baraza la Madiwani lililokutanisha Madiwani, Wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe pamoja na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Korogwe. Mhe. Bukhay alifafanua kuwa iwapo Watendaji wa Vijiji watashiriki ipasavyo katika kutatua migogoro ya ardhi inayojitokeza katika maeneo yao watasaidia kumaliza migogoro hiyo katika ngazi ya Vijiji.
“Maelekezo yote tumeyapokea na ninaimani kubwa Waheshimiwa Madiwani watashirikiana na Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Watendaji wa Vijiji katika kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo yao” alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Diwani wa Kata ya Mtonga. Mhe. Komba alifafanua kuwa Madiwani wataendelea kushirikiana na Watendaji wa Vijiji katika utatuzi wa migogoro ya ardhi ili kudumisha Amani na utulivu katika jamii.
“Mheshimiwa Kalist ametuonyesha dira ya utatuzi wa migogoro ya ardhi iliyopo katika jamii yetu. Viongozi iwapo watayafanyia kazi maelekezo yake, migogoro ya ardhi itapungua katika jamii” alisema Ndugu John Mapunda ambaye ni Mwananchi wa Mji wa Korogwe aliyeshiri katika Baraza la Madiwani la Papo kwa Papo kwa lengo la lufahamu shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.