Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh.Balozi Dkt. Batilda Burian amewataka Watumishi wa Serikali na wale wanaofanya kazi Sekta binafsi kufanya kazi kwa Nidhamu ,Uadilifu Haki na Utu ili kulinda heshima mahali pa kazi. Mh. Balozi Dkt. Batilda Burian ameyasema hayo kwenye Siku ya Wafanyakazi Mei mosi ambapo kimkoa siku hiyo ya Mei mosi ilifanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chanika Halmashauri ya Mji Handeni Mei 01, Mwaka huu (2025).
Pia Mh. Balozi Dktk. Batilda Burian amewaomba na kuwaagiza Waajiri na Viongozi wa Serikali kuhakikisha Maslahi ya Watumishi yanaboreshwa. Kwaupande mwingine amesisitiza Siku hii ya Wafanyakazi yaani Meimosi ilete tija na Mabadiliko kwa Watumishi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.