Wilaya ya Korogwe yafanya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
Wilaya ya Korogwe imeungna na Maeneo mengine hapa Nchini na Ulimwengu kwa ujumla katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani. Siku ambayo huadhimishwa Ulimwenguni kote kila ifikapo Mei 01, ya kila mwaka. Siku ya Wafanyakazi Duaniani mwaka huu Wilayani Korogwe iliadhimishwa kwa Wafanyakazi kushiriki katika Maandamano ya Wafanyakazi pamoja na Michezo mbalimbali. Maadhimisho hayo ya Siku ya Wanyakazi Duniani yalifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe (Korogwe TTC).
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Wilayani Korogwe yalishirikisha Viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi kutoka Sekta za Umma pamoja na Binafsi huku wakiwakilisha vyama vyao vya Wafanyakazi kikiwapo Chama cha CWT, TALGWU, TIPAU, TUGHE pamoja na Chama cha TUICO. Kauli mbiu ya Mwaka huu kwa hapa Nchini ni ”Mishahara na Maslahi bora kwa Wafanyakazi ndio kilio chetu, Kazi Iendelee”. Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ya Kiwilaya alikua Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi.
“Wakurugenzi wote, hakikisheni mnatatua changamoto za mafao ya likizo pamoja utoaji wa motisha za Wafanyakazi” alisema Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi wakati akizungumza na Wafanyakazi walioshiriki katika Siku ya Wafanyakazi Duniani katika Viwanja vya Korogwe TTC. Mhe. Mwanukuzi alifafanua kuwa pamoja na changamoto ndogondogo zilizopo katika maeneo ya kazi, Wafanyakazi ni vyema kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuimarisha mshikamo katika maeneo ya kazi.
“Tunatoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais kwa kuongeza jitihada za kutatua kero za Wafanyakazi hapa nchini”alisema Bi. Pilli Mdoe ambaye ni Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilayani Korogwe wakati akisoma Risala ya Siku ya Wafanyakazi Duniani katika Viwanja vya Korogwe TTC. Bi. Pilli alisisitiza kuwa anaimani kubwa salamu za kero za wafanyakazi hapa Nchi zitamfikia Mheshimiwa Rais na kero hizo atazipatia ufumbuzi katika kuhakikisha wafanyakazi wanaboreshewa maslahi bora katika maeneo ya kazi.
Katika hatua nyengine, Bi. Pili Mdoe alitoa pongezi kwa Viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa Vyama vyote vya Wafanyakazi kwa kushiriki katika Maadhimisho hayo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa ngazi ya Wilaya. Nao Wafanyakazi walioshiriki katika Maadhimisho hayo walitoa shukrani kwa Viongozi vya Vyama vya Wafanyakazi na Serikali kwa ujumla kwa kufanikisha Maadhimisho hayo yenye lengo la kuimarisha umoja na mshikamano wa Wafanyakazi katika kudai maslahi bora katika maeneo yao ya kazi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.