Wilaya ya Korogwe yazindua kampeni ya ugawaji wa vyandarua
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. Kissa Kasongwa akiwa pamoja na Mh. Mhandisi Mwanaasha Tumbo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza amezindua Kampeni ya ugawaji wa vyandarua bila malipo. Vyandarua hivyo vitagaiwa katika Halmashauri tatu ambazo ni Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Muheza. Uzinduzi wa kampani hiyo umefanyika Julai 24 mwaka huu katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Akizungumzizia mchakato huo wa ugawaji wa vyandarua Mh. Kissa Kasongwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe alisema “namshukuru Mh. Rais John Pombe Magufuli kwa kutuletea maendeleo katika sekta ya afya ikiwapo ugawaji vya vyandarua bila malipo kwa wananchi”. Mh. Kasongwa alifafanua kuwa ili vyandarua viweze kuwafikia walengwa waliokusudiwa lazima watakaoshiriki katika mchakato wa ugawaji wafanye kazi kwa uaminifu. Mh. Kasongwa alisisitiza kwa kusema “wagawaji wajiepushe na kujilimbikizia vyandarua kwa manufaa binafsi”.
Nae Ndugu Kasimu Kaoneka ambayye ni Afisa Elimu Shule za Msingi katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe anaemuakilisha Mkurugenzi alitoa shukrani kwa waandaaji wa Kampeni ya ugawaji wa vyandarua bila malipo katika Halmashauri zote tatu. Ndugu Kaoneka alitoa nasaha kwa watakaoshiriki katika Kampeni kwa kusema” kila mmoja katika eneo lake atekeleze majukumu yake ipasavyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali”.
Nae Bi. Leah Ndekuka ambaye ni Afisa kutoka Wizara ya Afya katika Kitengo cha Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria alisema “Lengo la Kampeni hii ya ugawaji wa vyandarua bila malipo ni kuhakikisha kuwa vyandarua vinawafikia wananchi wengi ili kutimiza miikakati ya Serikali katika kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2030 ugonjwa wa Malaria tumeutokomeza hapa nchini". Bi. Leah alisisitiza kuwa Kampeni hii nimuendelezo wa Mikakati ya Wizara ya Afya katika kukakikisha inafikia Halmashauri takribani Hamsini (50) zilizopo kwenye Mikoa kumi hapa nchini”.
Kwa upande mwingine Bi. Hilda Mgomapayo ambaye ni mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alisisitiza kuwa ili Kampeni hii iweze kuwafikia wananchi kwa haraka, viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuwaelimisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua. Bi. Hilda alisema “nawaomba viongozi wa dini mtusaidie kufikisha ujumbe kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua”.
Nae Dr. Heri Kilwale ambaye ni Mratibu wa Malaria kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema “tunatarajia Kampeni hii ya ugawaji wa vyandarua itachukua takribani wiki mbili mpaka kumalizika” Dr. Kilwale alifafanua kuwa katika Mji wa Korogwe Kampeni hii itahusisha Kata zote kumi moja. Kwaupande wa viongozo wa dini, Ndugu Abas Makamba ambaye ni Sheikh kutoka Kata ya Magoma iliyopo Wilaya ya Korogwe alisema “tunaishukuru serikali kwa kuandaa Kampeni hii ya ugawaji wa vyandarua bila malipo ili kupambana na ugonjwa wa Malaria”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.