Zoezi la Kliniki ya Ardhi Halmashauri ya Mji wa Korogwe limehitimishwa rasmi Siku ya Jumanne Agosti 12, 2025 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi Manundu. Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Tanga Bw. Jabir Singano alitoa wito kwa Wananchi wa Korogwe kufuata Sheria Kanuni na Miongozo inayotolewa na Serikali chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kuepusha migogoro ya Ardhi isiyokuwa ya lazima. Bw. Singano alitoa kauli hiyo Siku ya Jumanne Agosti 12, 2025 katika Viwanja vya Shule ya Msingi wakati wa kuhitimisha Kliniki ya Ardhi. Jumla ya Wananchi 112 wamehudumiwa na kupatiwa Elimu kuhusu Masuala ya Ardhi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.