Maafisa uandikishaji ngazi ya Kata waapishwa
Maafisa uandikishaji ngazi ya Kata katika Jimbo la Korogwe Mjini wameapishwa na kupewa mafunzo ya namna ya usimamizi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwaajili ya uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba 2025. Maafisa uandikishaji hao kutoka Kata 11 zilizopo katika Jimbo la Korogwe Mjini waliapa mbele ya Mhe. Sikitu Mwalusamba ambaye ni Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Korogwe. Kiapo hicho pamoja na mafunzo kilifanyika Februari 6, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mafuzo yanatarajiwa kufanyika kwa Siku Mbili kuanzia Februari 6 hadi 7, 2025.
Mafunzo ya uboreshji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa Maafisa uandikishaji ngazi ya Kata yameratibiwa na Afisa Mwandikishaji Msaidizi Jimbo la Korogwe Mjini kwa kushirikiana na Maafisa kutoka Tume huru ya Taifa ya uchaguzi nchini Tanzania.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.