Madiwani wa Mji wa Korogwe wapongezwa kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi ametoa pongezi kwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Utekelezaji huo wa Ilani ya CCM umehusisha ushiriki wa Madiwani katika Ujenzi wa Miradi ya maendeleo pamoja na utatuzi wa kero za Wananchi. Pongezi hizo zimetolewa wakati cha Kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya Kwanza katika Mwaka wa fedha 2022/23 kilichofanyika Novemba 2, Mwaka huu katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Natoa pongezi kwa Waheshimiwa Madiwani kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ikiwemo ushiriki wenu katika Ujenzi wa Miradi ya maendeleo pamoja na utatuzi wa kero za wananchi” alisema Mhe. Basilla Mwanukuzi ambanye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe. Mhe. Basilla alifafanua kuwa ni vyema Madiwani wakashiriki katika Ujenzi wa Miradi ya maendeleo kama vile elimu na afya katika kwa lengo la kuhakikisha Wananchi wanapata huduma za jamii jirani na maeneo yao.
Katika hatua nyengime, Mhe. Basilla Mwanukuzi amewataka Madiwani wa Mji wa Korogwe kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki katika kuwafichua watu wote wanaojihusisha na biashara ya mihadarati katika maeneo yao ili kunusuru vijana wasiangamie katika uraibu wa mihadarati kwa kuwa ndio tegemezi kwa ujenzi wa Taifa letu. Mhe.Basilla alisema “Waheshimiwa Madiwani naomba tushirikiane katika kuwafichua watu wote wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya katika maeneo yetu”.
Kwa upande mwengine, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kushiriki vyema katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ili kupata fedha za kutosha zikazotumika katika Ujezi wa Miradi mbalimbali ya maendeleo Mhe. Komba alisema “Wakuu wa Idara na Vitengo kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki ipasavyao katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri”.
“Maagizo yote yaliyotolewa katika Baraza la Madiwani tumeyapokea na tutayafanyia kazi” alisema Bw. Nicodemus Bei ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashuri ya Mji wa Korogwe wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani . Nae Ndugu Maurice Kinyashi ambaye ni Mwananchi wa Mji wa Korogwe aliyeshiriki katika Kikao cha Baraza la Madiwani alitoa pongenzi kwa Baraza hilo la Madiwani jinsi lilivojadili kwa kina changamoto mbalimbali zilizopo katika Jamii.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.