Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Lengo la ziara ya Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kufungua miradi mbalimbali iliyokuwa inatekelezwa na Serikali kwa baadhi ya Halamshauri hizo pia Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameongea na Wananchi wa Mji wa Korogwe amewataka kila Mwananchi ajiandikishe kwenye Daftari la kudumu la mpiga kura ili apate sifa ya kumchagua kiongozi anayemtaka kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba, 2025 mwaka huu . Mh Rais ameyasema hayo kwenye Viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe (TTC) Mkoani Tanga Febuari 24, 2025.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.