Mji wa Korogwe wapanda miti kuuadhimisha Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Kuelekea Miaka 59 ya Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ifikapo Aprili 26, Mwaka huu. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe akiambatana na Watumishi wa Halmashauri hiyo, wameshiriki katika zoezi la upandaji wa Miti pamoja na Usafi wa Mazingira katika Shule ya Sekondari ya New Bagamoyo iliyopo Kata ya Bagamoyo. Zoezi hilo la upandaji wa Miti pamoja na Usafi wa Mazingira limefanyika Aprili 25, Mwaka huu.
Kauli Mbiu ya Mwaka huu; Miaka 59 ya Muungano, “Umoja na Mshikamano ndiyo Nguzo ya Kukuza Uchumi Wetu”
“Pamoja na kutekeleza agizo la upandaji Miti na Usafi wa Mazingira katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, upandaji Miti na Usafi wa Mazingira ni zoezi tunalotekeleza kila siku na litakuwa endelevu kwa ustawi wa Mji wetu wa Korogwe” alisema Bw. Burhani Ngulungu ambaye ni Afisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe anayemwakilisha Mkurugenzi katika zoezi la upandaji wa Miti na Usafi wa Mazingira. Bw. Burhani alisisitiza kuwa jukumu la Uhifadhi na Usafi wa Mazingira sio la Serikali pekeyeke bali kila Mwananchi anapaswa kuwajibika katika zoezi hilo.
Katika Hatua Nyengine, Mkuu wa Shule ya Sekondari New Bagamoyo, Walimu na Wanafunzi kwa ujumla walitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Watumishi wote walioshiriki katika zoezi la upandaji wa Miti pamoja na Usafi wa Mazingira katika shule hiyo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.