Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe atembelea ujenzi wa miradi ya maendeleo
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Happy Luteganya akiambatana pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo ametembelea ujenzi wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu ili kujionea utekelezaji wa miradi hiyo. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Mtonga pamoja na Matondoro. Ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kata ya Majengo, Ujenzi wa bweni shule ya sekondari Ngombezi pamoja na Ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya sekondari Msambiazi. Ziara hiyo ilifanyika Desemba 12, Mwaka huu (2024) katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.