Mradi wa ujenzi wa mtambo wa maji taka wakamilika
Mradi wa Ujenzi wa Mtambo wa kuchakata Maji Taka uliopo katika Kata ya Bagamoyo Mjini Korogwe umekamilika kwa Asilimia Mia Moja. Mradi huo wenye Thamani ya Shilingi Milioni 247 uliofadhiliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Borda kutoka Nchini Ujerumani. Taasisi ya Borda pamoja na kufadhili Ujenzi wa Mtambo wa Maji Taka pia wamefadhili Gari la kubebea Maji Taka lenye Thamani ya Shilingi Milioni 60, Gari hilo litasaidia kutoa huduma ya kubeba Maji Taka katika Mji wa Korogwe kwa gharama nafuu.
Taarifa ya kukamilika kwa mradi huo ilitolewa katika Kikao Maalumu kilichoitishwa na Taasisi ya Borda kwa lengo la kutoa Taarifa rasmi kwa Madiwani wa Mji wa Korogwe, Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ya HTM. Baada ya Mradi huo kukamilika, Mtambo wa kuchakata Maji Taka utakuwa chini ya usimamizi wa HTM. Kikao hicho cha utoaji wa Taarifa kilifanyika Septemba 25, Mwaka huu (2024) Katika ukumbi wa Mikutano wa Mvuni Hotel.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.