Viongozi wa dini, siasa watakiwa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
Afisa Mwandikishaji Msaidizi wa Jimbo la Korogwe Mjini Bw. Elinlaa Kivaya amewataka viongozi wa Dini pamoja na Viongozi wa Siasa kuhamasisha Wananchi wajitokeze kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba, Mwaka huu (2025). Bw. Kivaya alitoa kauli hiyo wakati wa Kikao cha siku moja kilichokutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili namna ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura katika Jimbo la Korogwe Mjini. Kikao hicho kilifanyika Februari 5, Mwaka huu (2025) katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Zoezi la uboreshaji wa dafatari la wapiga kura katika Jimbo la Korogwe Mjini linatarajiwa kuanza Februari 13, na litakamilika Februari 19 Mwaka huu (2025). Vituo vyote vitafunguliwa kuanzia Saa 2: 00 Asubuhi na vitafungwa Saa 12:00 Jioni.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.