Wafanyakazi wa Viwandani wajitokeza kwa wingi kupata Chanjo ya Uviko -19
Wafanyakazi kutoka Kiwanda cha Winafr Co. Ltd pamoja na Kiwanda cha Cyreka East Africa Dev. Co. Ltd vinavyojihusisha na uchakataji wa nyuzi za mkonge vilivyopo Mji wa Korogwe wamejitokea kwa wingi kupata Chanjo ya Uviko -19 ili kuimarisha kinga za mwili na ziweze kupambana na Ugonjwa kwa Uviko -19.
Mwitikio huo wa Wafanyakazi kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo umetokana na Timu ya Kampeni ya Mpango Harakishi na Shirikishi wa Chanjo ya Uviko -19 kuwatembelea Wafanyakazi wa Viwandani na Uongozi kwa ujumla kwa lengo la kuwaelimisha na kuwahamasisha ili waweze kupata Chanjo. Timu ya Kampeni ya Chanjo ilitembelea Viwandani kwa Siku Mbili mfululizo kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 01, mwaka huu ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya utoaji wa Chanjo ya Uviko -19 Nyumba kwa Nyumba.
“Pamoja na changamoto ndogondogo za hofu walizokuwa nazo Wafanyakazi lakini muitikio wao wa kupata channjo ni mkubwa” alisema Ndugu Jumanne Huruka ambaye Afisa Afya katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe na ndie Kiongozi wa Timu ya Kampeni ya Uviko -19 Viwandani. Ndugu Huruka alifafanua kuwa hofu walizonazo Wafanyakazi ni maneno ya mtaani ambayo hayana ukweli wowote. Ndugu Huruka aliendelea kufafanua kwa msisitizo na kusema “Chanjo ya Uviko -19 ni salama kabisa na haina athari yoyote katika mwili wa mwanadamu”
“Natoa wito kwa vijana wenzangu wajitokeze kwa wingi kupata Chanjo, Chanjo hii ni kama Chanjo nyengine haina maumivu wakati wa kuchanja kama wanavyohisi” alisema Ndugu Msafiri Masudi akiwa na furaha kubwa baada ya kupata Chanjo ya Uviko -19. Katika hatua nyengine, Ndugu Masudi alitoa shukrani kwa Timu ya Kampeni ya Chanjo kwa kuwapatia elimu ya kutosha Wafanyakazi wa Viwandani juu ya umuhimu wa Chanjo ya Uviko -19 hadi wakahamasika na kuamua kuchanja.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.