Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu, Watendaji na Waganga wafawidhi wapigwa Msasa masuala ya kutumia Mfumo wa Manunuzi wa Serikali ( NesT).
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Burhan Ngulungu amewataka Wataalamu walioshiriki Mafunzo hayo kuzingatia kanuni na miongozo ya Utumishi wa umma wakati wa kufanya Manunuzi ya Serikali. Lengo kuu ya Mafunzo hayo ni kuwapatia Uwezo na ujuzi wa Jinsi Watumishi wa Serikali watakavyofanya manunuzi kupitia Mfumo huo yaani (NesT).
Mafunzo hayo ya kuwajengea ujuzi Watumishi wa Serikali yalifanyika Aprili 03, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Washiriki wapatao Mia moja Hamsini (150) pia Mafunzo hayo yanatarajia kufanyika kwa Siku mbili katika Ukumbi wa Halamashauri ya Mji wa Korogwe kuanzia Aprili 03, 2025 hadi Aprili 04, 2025.
Naye .”Bi. Nuru Bazaar ambaye ni Mkufunzi wa Mafunzo kwa Watumishi waliohudhuria Mafunzo alisema ,”Manunuzi yote ya Serikali yatafanyika kupitia Mfumo wa Manunuzi yaani (NesT) na sivyo vinginevyo kwa hiyo amewataka Washiriki mafunzo kuzingatia miongozo pamoja na Kanuni
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.