Wanafunzi 19,417 wanatarajiwa kupatiwa kingatiba ya ugojwa wa minyoo na kichocho
Halmashauri ya Mji wa Korogwe chini ya Mpango wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele inatarajia Novemba 22 hadi 23, Mwaka huu kutoa Kingatiba za ugojwa wa Minyoo na Kichocho kwa Wanafuzi wa Shule za Msingi takribani 19,417. Idadi hiyo ya Wananfunzi itahusisha Wanafunzi wenye umri kuanzia miaka Mitano hadi Kumi na Nne kutoka Shule za Msingi 35 za Serikalini pamoja na Binafsi. Mpango huo wa utoaji wa Kingatiba ulitangazwa wakati wa Kikao Kazi cha Wataalamu wa afya kilichofanyika Novemba 19, Mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Hospitali ya Mji wa Korogwe (Magunga).
“Serikali imejipanga vyema kuhakikisha ugojwa wa Minyoo na Kichocho unapungua au kutokomezwa kabisa katika shule za msingi hapa nchini” alisema Bi. Florence Makunda ambaye ni Mfamasia na Mratibu wa utoaji Kingatiba za ugojwa wa Minyoo na Kichocho kutoka Wizara ya Afya. Bi. Florence asisitiza kuwa suala la uhamasishaji wa unywaji wa Kingatiba (Dawa) kwa Wanafunzi sio la Serikali pekeyake, bali Wazazi na Walezi pia wanatakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Wanafunzi wote wamekwenda shule siku ya utoaji Kingatiba.
“Kingatiba zitakazotolewa kwa Wanafunzi ni salama na hazina madhara yoyote” alisema Bi. Veronica Joseph ambaye ni Mratibu wa Magojwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe aliyemuakilisha Mkurugenzi katika Kikao Kazi cha Wataalamu wa afya. Bi, Veronica alifafanua kuwa Kingatiba zitakazotolewa kwa Wanafunzi shuleni ni pamoja na Albendazole na Praziquantel. Nae Bw. Aseri Mshana ambaye ni Muakilishi kutoka Idara ya Elimu ya Awali na Msingi Katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema “Walimu wako tayari kwa utekelezaji wa zoezi la utoaji wa kingatiba kwa Wanafuzi”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.