Wananchi wa Korogwe wachangia Maoni katika Mpango wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 - 2050
Wananchi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe na Mji wa Korogwe wamejitokeza kwa wingi katika Kikao cha kuchangia Maoni yao katika Mpango wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 - 2050. Kikao hicho kiliwakutanisha Wananchi kutoka Makundi mbalimbali ili kutoa Maoni yao juu ya Tanzania waitakayo kwa Miaka ya baadae. Kikao hicho kilifanyika Julai 23, Mwaka huu (2024) katika Ukumbi wa Halmshauri ya Mji wa Korogwe na Mgeni rasmi katika kikao hicho alikua Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema.
Katika Kikao hicho Wananchi wa Korogwe walitoa Maoni mbalimbali juu Tanzania waitakayo kwa Miaka ya baadae. Miongoni mwa Maoni yao katika Mpango wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 - 20250 ni Pamoja na kuwe na Mpango wa: Kupambana na Majanga, Kuimarisha Amani na Utulivu, Siasa Safi na Uongozi Bora, Kuwekeza katika Kilimo cha Kisasa, Mpango bora wa Matumizi ya Ardhi, Kuwekeza katika Viwanda vya uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali, Kukomesha Ushoga, Usagaji na Ubakaji, na Kudumisha Utamaduni, Mila na Desturi zetu.
“Nanawashukuru Ndugu zangu wote wa Korogwe mliohudhuria katika Kikao, Maoni yote mliyochangia yanatija katika Taifa letu” alisema Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema. Mhe. Mwakilema alisistiza kuwa Serikali itayafanyia kazi Maoni yote ya Wananchi ili kuwa na Mpango wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 - 2050 ulioshirikisha Wananchi Wote.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.