Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Happy Luteganya akiambatana na Wanawake wa Wilaya ya Korogwe wametoa zawadi kwa Wanafunzi wenye Ulemavu wa Akili na Usonji zawadi hizo zimetolewa kwa Shule mbili ikiwemo Shule ya Msingi kwamngumi na Shule ya Msingi kwasemangube pia wametoa mahitaji katika Hospitali ya Mji wa Korogwe Magunga. Lengo la ziara hii ni kuunga mkono jitihada za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikia Wanawake na Watoto wenye changamoto ya Uhitaji ni katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kitaifa Maadhimisho hayo yanatarajia kufanyika Mkoani Arusha na Kiwilaya yanatarajia kufanyika Machi 05 ,2025 kata ya Makuyuni Wilaya ya Korogwe. Ziara hiyo imefanyika Machi 4, 2025.
Mahitaji yaliyotolewa na kukabidhiwa Wanafunzi wenye Ulemavu wa Akili ,Usonji Pamoja na Wagonjwa waliolazwa ni Pamoja na Mchele, Sukari, Juisi, Sabuni za kufulia na za kuogea, Tambi, Biskuti , pipi na Penseli.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.