Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Elinlaa Kivaya ameshiriki zoezi la upandaji miti Pamoja na Watumishi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Zoezi la Upandaji Miti limefanyika katika Shule Mpya ya Sekondari Majengo na jumla ya miti Mia mbili (200) imepandwa.
Lengo kuu la Zoezi la Upandaji Miti lilikuwa ni kuungana na Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Aprili 26, 1964. Zoezi la upandaji miti lilifanyika katika Shule Mpya ya Sekondari Majengo Aprili 26, Mwaka huu (2025). Na kauli mbiu ya Mwaka huu ya Siku ya Maadhimisho ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema”Miaka Sitini na Moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Muungano wetu ni dhamana, Heshima na tunu ya Taifa letu, Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.